6Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya dunia,’ nayo manyunyu ya mvua, ‘Uwe mvua ya nguvu.’
7Ili wanadamu wote aliowaumba wapate kujua kazi zake, yeye humzuilia kila mtu shughuli zake.
8Wanyama hujificha; hubakia kwenye mapango yao.
9Dhoruba hutoka katika chumba chake, baridi hutoka katika upepo uendao kasi.
10Pumzi ya Mungu hutoa barafu, eneo kubwa la maji huganda.