11Huyasheheneza mawingu kwa maji, naye husambaza umeme wake wa radi kupitia hayo.
12Nayo mawingu huzungukazunguka pande zote kwa amri yake, juu ya uso wa dunia yote, kufanya lolote ayaamuruyo.
13Huleta mawingu ili kuadhibu wanadamu, au kuinyeshea dunia yake na kuonyesha upendo wake.
14“Ayubu, sikiliza hili; nyamaza na uyafikiri maajabu ya Mungu.
15Je, unajua jinsi Mungu anavyoyaongoza mawingu, na kufanya umeme wake wa radi utoe mwanga?