15Waovu huzuiliwa nuru yao, nao mkono wao ulioinuliwa huvunjwa.
16“Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari? Au kutembea mahali pa ndani pa vilindi?
17Umewahi kuonyeshwa malango ya mauti? Umewahi kuiona milango ya uvuli wa mauti?
18Je, wewe unafahamu ukubwa wa dunia? Niambie kama unajua haya yote.
19“Njia ya kufika kwenye makao ya nuru ni ipi? Nako maskani mwa giza ni wapi?