29Barafu inatoka tumbo la nani? Ni nani azaaye ukungu kutoka mbinguni,
30wakati maji yawapo magumu kama jiwe, wakati uso wa vilindi vya maji unapoganda?
31“Je, waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia? Waweza kulegeza kamba za Orioni?
32Waweza kuyaongoza makundi ya nyota kwa majira yake, au kuongoza Dubu na watoto wake?
33Je, unajua sheria zinazotawala mbingu? Waweza kuweka utawala wa Mungu duniani?