3Ndipo Ayubu akamjibu Bwana:
4“Mimi sistahili kabisa: ninawezaje kukujibu wewe? Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu.
5Nimesema mara moja, lakini sina jibu; naam, nimesema mara mbili, lakini sitasema tena.”
6Ndipo Bwana akasema na Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli:
7“Jikaze kama mwanaume; nitakuuliza maswali, nawe yakupasa unijibu.