5Nimesema mara moja, lakini sina jibu; naam, nimesema mara mbili, lakini sitasema tena.”
6Ndipo Bwana akasema na Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli:
7“Jikaze kama mwanaume; nitakuuliza maswali, nawe yakupasa unijibu.
8“Je, utabatilisha hukumu yangu? Utanilaumu mimi ili kujihesabia haki mwenyewe?
9Je, una mkono kama wa Mungu, nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama yake?