16Kwa hiyo maskini analo tarajio, nao udhalimu hufumba kinywa chake.
17“Heri mtu yule ambaye Mungu humrudi; kwa hiyo usidharau adhabu yake Mwenyezi.
18Kwa kuwa hutia jeraha, lakini pia huyafunga; huumiza, lakini mikono yake pia huponya.
19Kutoka majanga sita atakuokoa; naam, hata katika saba hakuna dhara litakalokupata wewe.
20Wakati wa njaa atakukomboa wewe na kifo, naye katika vita atakukomboa na pigo la upanga.