Ayubu 5

Wakati wa njaa atakukomboa wewe na kifo, naye katika vita atakukomboa na pigo la upanga.

Job 5:20 (UKJV) In famine he shall redeem you from death: and in war from the power of the sword.

18Kwa kuwa hutia jeraha, lakini pia huyafunga; huumiza, lakini mikono yake pia huponya.

19Kutoka majanga sita atakuokoa; naam, hata katika saba hakuna dhara litakalokupata wewe.

20Wakati wa njaa atakukomboa wewe na kifo, naye katika vita atakukomboa na pigo la upanga.

21Utalindwa kutokana na kichapo cha ulimi, wala hutakuwa na sababu ya kuogopa maangamizi yatakapokujia.

22Utayacheka maangamizo na njaa, wala hutakuwa na sababu ya kuwaogopa wanyama wakali wa mwituni.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.