15hivyo ninachagua kujinyonga na kufa, kuliko huu mwili wangu.
16Ninayachukia maisha yangu; nisingetamani kuendelea kuishi. Niache; siku zangu ni ubatili.
17“Mwanadamu ni kitu gani hata umjali kiasi hiki, kwamba unamtia sana maanani,
18kwamba unamwangalia kila asubuhi na kumjaribu kila wakati?
19Je, hutaacha kamwe kunitazama, au kuniacha japo kwa kitambo kidogo tu?