Ayubu 7

Je, hutaacha kamwe kunitazama, au kuniacha japo kwa kitambo kidogo tu?

Job 7:19 (UKJV) How long will you not depart from me, nor let me alone till I swallow down my spittle?

17“Mwanadamu ni kitu gani hata umjali kiasi hiki, kwamba unamtia sana maanani,

18kwamba unamwangalia kila asubuhi na kumjaribu kila wakati?

19Je, hutaacha kamwe kunitazama, au kuniacha japo kwa kitambo kidogo tu?

20Ikiwa nimetenda dhambi, nimekufanyia nini, Ewe mlinzi wa wanadamu? Kwa nini umeniweka niwe shabaha yako? Je, nimekuwa mzigo kwako?

21Kwa nini husamehi makosa yangu na kuachilia dhambi zangu? Kwa kuwa hivi karibuni nitalala mavumbini; nawe utanitafuta, wala sitakuwepo.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.