16Ninayachukia maisha yangu; nisingetamani kuendelea kuishi. Niache; siku zangu ni ubatili.
17“Mwanadamu ni kitu gani hata umjali kiasi hiki, kwamba unamtia sana maanani,
18kwamba unamwangalia kila asubuhi na kumjaribu kila wakati?
19Je, hutaacha kamwe kunitazama, au kuniacha japo kwa kitambo kidogo tu?
20Ikiwa nimetenda dhambi, nimekufanyia nini, Ewe mlinzi wa wanadamu? Kwa nini umeniweka niwe shabaha yako? Je, nimekuwa mzigo kwako?