4Hekima yake ni kubwa sana na ana uwezo mwingi mno. Ni nani aliyempinga naye akawa salama?
5Aiondoa milima bila yenyewe kujua na kuipindua kwa hasira yake.
6Aitikisa dunia kutoka mahali pake na kuzifanya nguzo zake zitetemeke.
7Husema na jua, nalo likaacha kuangaza; naye huizima mianga ya nyota.
8Yeye peke yake huzitandaza mbingu na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.