6Aitikisa dunia kutoka mahali pake na kuzifanya nguzo zake zitetemeke.
7Husema na jua, nalo likaacha kuangaza; naye huizima mianga ya nyota.
8Yeye peke yake huzitandaza mbingu na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.
9Yeye ndiye Muumba wa nyota za Dubu, na Orioni, Kilimia, na makundi ya nyota za kusini.
10Hutenda maajabu yasiyopimika, miujiza isiyoweza kuhesabiwa.