12Alipokuwa akiingia kwenye kijiji kimoja, watu kumi waliokuwa na ukoma wakakutana naye. Wakasimama mbali,
13wakapaza sauti, wakasema, “Yesu, Bwana, tuhurumie!”
14Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” Nao walipokuwa njiani wakienda, wakatakasika.
15Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa Yesu, akimsifu Mungu kwa sauti kuu.
16Akajitupa miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikuwa Msamaria.