14Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” Nao walipokuwa njiani wakienda, wakatakasika.
15Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa Yesu, akimsifu Mungu kwa sauti kuu.
16Akajitupa miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikuwa Msamaria.
17Yesu akauliza, “Je, hawakutakaswa wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa?
18Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumshukuru Mungu isipokuwa huyu mgeni?”