11Yoyada alikuwa baba wa Yonathani, na Yonathani alikuwa baba wa Yadua.
12Katika siku za Yoyakimu, kulikuwa na wakuu wa jamaa za kikuhani: wa jamaa ya Seraya, Meraya; wa jamaa ya Yeremia, Hanania;
13wa jamaa ya Ezra, Meshulamu; wa jamaa ya Amaria, Yehohanani;
14wa jamaa ya Maluki, Yonathani; wa jamaa ya Shebania, Yosefu;
15wa jamaa ya Harimu, Adna; wa jamaa ya Meremothi, Helkai;