16“Bwana, Mungu wa roho zote za wanadamu, na amteue mtu juu ya jumuiya hii
17ili atoke na kuingia mbele yao, atakayewaongoza katika kutoka kwao na kuingia kwao, ili watu wa Bwana wasiwe kama kondoo wasio na mchungaji.”
18Kwa hiyo Bwana akamwambia Mose, “Mchukue Yoshua mwana wa Nuni, mtu ambaye Roho yuko ndani yake, uweke mkono juu yake.
19Msimamishe mbele ya kuhani Eleazari pamoja na kusanyiko lote, umpe maagizo mbele yao.
20Mpe sehemu ya mamlaka yako ili jumuiya yote ya Waisraeli ipate kumtii.