14Njoo ushirikiane nasi, vitu vyote tutakavyopata tutagawana.”
15Mwanangu, usiandamane nao. Usiweke mguu wako katika njia zao,
16kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi, ni wepesi kumwaga damu.
17Tazama ni jinsi gani ilivyo kazi bure kutandaza wavu wakati ndege wote wanakuona!
18Watu hawa huvizia kumwaga damu yao wenyewe; hujivizia tu wenyewe!