1Bwana huchukia sana mizani za udanganyifu, bali vipimo sahihi ni furaha yake.
2Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu, bali unyenyekevu huja na hekima.
3Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.
4Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu, bali haki huokoa kutoka mautini.