2Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu, bali unyenyekevu huja na hekima.
3Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.
4Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu, bali haki huokoa kutoka mautini.
5Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyonyooka, bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe.
6Haki ya wanyofu huwaokoa, bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya.