4Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu, bali haki huokoa kutoka mautini.
5Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyonyooka, bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe.
6Haki ya wanyofu huwaokoa, bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya.
7Wakati mtu mwovu anapokufa, matumaini yake hutoweka; yote aliyoyatazamia kutokana na nguvu zake huwa si kitu.
8Mtu mwenye haki huokolewa kutoka taabu, naye mtu mwovu huingia humo badala yake.