25Mtu mkarimu atastawi; yeye awaburudishaye wengine ataburudishwa mwenyewe.
26Watu humlaani mtu awanyimae watu nafaka, bali baraka itamkalia kichwani kama taji yeye aliye radhi kuiuza.
27Yeye atafutaye mema hupata ukarimu, bali ubaya huja kwake yeye autafutaye.
28Yeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka, bali mwenye haki atastawi kama jani bichi.
29Yeye aletaye taabu kwa jamaa yake atarithi tu upepo, naye mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye hekima.