27Yeye atafutaye mema hupata ukarimu, bali ubaya huja kwake yeye autafutaye.
28Yeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka, bali mwenye haki atastawi kama jani bichi.
29Yeye aletaye taabu kwa jamaa yake atarithi tu upepo, naye mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye hekima.
30Tunda la mwenye haki ni mti wa uzima, naye mwenye hekima huvuta roho za watu.
31Kama wenye haki watapokea ujira wao duniani, si zaidi sana yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi?