Mithali 16

Moyo wa mtu mwenye hekima huongoza kinywa chake, na midomo yake huchochea mafundisho.

Proverbs 16:23 (UKJV) The heart of the wise teaches his mouth, and adds learning to his lips.

21Wenye hekima moyoni huitwa wenye ufahamu, na maneno ya kupendeza huchochea mafundisho.

22Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwa wale walio nao, bali upumbavu huleta adhabu kwa wapumbavu.

23Moyo wa mtu mwenye hekima huongoza kinywa chake, na midomo yake huchochea mafundisho.

24Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali, ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa.

25Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, bali mwisho wake huelekeza mautini.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.