23Moyo wa mtu mwenye hekima huongoza kinywa chake, na midomo yake huchochea mafundisho.
24Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali, ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa.
25Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, bali mwisho wake huelekeza mautini.
26Shauku ya mfanyakazi humhimiza kufanya kazi; njaa yake humsukuma aendelee.
27Mtu mbaya kabisa hupanga mabaya, maneno yake ni kama moto uunguzao.