25Ni mtego kwa mtu kuweka wakfu kitu kwa haraka na baada ya kitambo kidogo kufikiria tena nadhiri zake.
26Mfalme mwenye hekima hupepeta waovu, hulipitisha gurudumu la kupuria juu yao.
27Taa ya Bwana huchunguza roho ya mwanadamu, huchunguza utu wake wa ndani.
28Upendo na uaminifu humweka mfalme salama, kwa njia ya upendo, kiti chake cha enzi huwa salama.
29Utukufu wa vijana ni nguvu zao, mvi ni fahari ya uzee.