19Sikiliza, mwanangu na uwe na hekima, weka moyo wako kwenye njia iliyo sawa.
20Usiwe miongoni mwa wanywao mvinyo, au wale walao nyama kwa pupa,
21kwa maana walevi na walafi huwa maskini, nako kusinzia huwavika matambara.
22Msikilize baba yako, aliyekuzaa, wala usimdharau mama yako atakapokuwa mzee.
23Nunua kweli wala usiiuze, pata hekima, adabu na ufahamu.