15Usivizie kama haramia afanyavyo ili kuyashambulia makao ya mwenye haki, wala usiyavamie makazi yake,
16Kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena, lakini waovu huangushwa chini na maafa.
17Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo; wakati ajikwaapo, usiruhusu moyo wako ushangilie.
18Bwana asije akaona na kuchukia akaiondoa ghadhabu yake mbali naye.
19Usikasirike kwa sababu ya watu wabaya wala usiwaonee wivu waovu,