17Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo; wakati ajikwaapo, usiruhusu moyo wako ushangilie.
18Bwana asije akaona na kuchukia akaiondoa ghadhabu yake mbali naye.
19Usikasirike kwa sababu ya watu wabaya wala usiwaonee wivu waovu,
20kwa maana mtu mbaya hana tumaini la siku zijazo, nayo taa ya waovu itazimwa.
21Mwanangu, mche Bwana na mfalme, wala usijiunge na waasi,