27Maliza kazi zako za nje, nawe uweke mashamba yako tayari, baada ya hayo, jenga nyumba yako.
28Usishuhudie dhidi ya jirani yako bila sababu, au kutumia midomo yako kudanganya.
29Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; nitamlipiza mtu yule kwa kile alichonitendea.”
30Nilipita karibu na shamba la mvivu, karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili,
31miiba ilikuwa imeota kila mahali, ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka.