11Mpumbavu huonyesha hasira yake yote, bali mwenye hekima hujizuia.
12Kama mtawala akisikiliza uongo, maafisa wake wote huwa waovu.
13Mtu maskini na mtu anayeonea wanafanana kwa jambo hili: Bwana hutia nuru macho yao wote wawili.
14Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki, kiti chake cha enzi kitakuwa thabiti siku zote.
15Fimbo ya maonyo hutia hekima, bali mtoto aliyeachiwa bila maonyo humwaibisha mama yake.