23Kiburi cha mtu humshusha, bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu hupata heshima.
24Anayekubaliana na mwizi ni adui wa nafsi yake mwenyewe; huapishwa lakini hathubutu kushuhudia.
25Kuwaogopa watu huwa ni mtego, bali yeyote amtumainiaye Bwana atakuwa salama.
26Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala, bali mtu hupata haki kutoka kwa Bwana.
27Mwenye haki huwachukia sana wasio waaminifu; waovu huwachukia sana wenye haki.