Mithali 30

“Mimi ni mjinga kuliko wanadamu wote; sina ufahamu wa kibinadamu.

Proverbs 30:2 (UKJV) Surely I am more brutish than any man, and have not the understanding of a man.

1Misemo ya Aguri mwana wa Yake, usia: Huyu mtu alimwambia Ithieli, naam, kwa Ithieli na kwa Ukali:

2“Mimi ni mjinga kuliko wanadamu wote; sina ufahamu wa kibinadamu.

3Sijajifunza hekima, wala sina maarifa ya kumjua yeye Aliye Mtakatifu.

4Ni nani ameshapanda mbinguni na kushuka? Ni nani ameshakusanya upepo kwenye vitanga vya mikono yake? Ni nani ameshafungia maji kwenye nguo yake? Ni nani ameimarisha miisho yote ya dunia? Jina lake ni nani, na mwanawe anaitwa nani? Niambie kama unajua!

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.