21“Kwa mambo matatu nchi hutetemeka, naam, kwa mambo manne haiwezi kuvumilia:
22Mtumwa awapo mfalme, mpumbavu ashibapo chakula,
23mwanamke asiyependwa aolewapo, naye mtumishi wa kike achukuapo nafasi ya bibi yake.
24“Vitu vinne duniani vilivyo vidogo, lakini vina akili nyingi sana:
25Mchwa ni viumbe wenye nguvu ndogo, hata hivyo hujiwekea akiba ya chakula chao wakati wa kiangazi.