8Alikuwa akishuka njiani karibu na pembe ya kwake, akielekea kwenye nyumba ya huyo mwanamke
9wakati wa machweo, jua likipungua nuru yake, giza la usiku lilipokuwa likiingia.
10Ndipo huyo mwanamke akatoka kumlaki, hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya udanganyifu.
11(Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi, miguu yake haitulii nyumbani;
12mara kwenye barabara za mji, mara kwenye viwanja vikubwa, kwenye kila pembe huvizia.)