10Ndipo huyo mwanamke akatoka kumlaki, hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya udanganyifu.
11(Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi, miguu yake haitulii nyumbani;
12mara kwenye barabara za mji, mara kwenye viwanja vikubwa, kwenye kila pembe huvizia.)
13Huyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu, na kwa uso usio na haya akamwambia:
14“Nina sadaka za amani nyumbani; leo nimetimiza nadhiri zangu.