12mara kwenye barabara za mji, mara kwenye viwanja vikubwa, kwenye kila pembe huvizia.)
13Huyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu, na kwa uso usio na haya akamwambia:
14“Nina sadaka za amani nyumbani; leo nimetimiza nadhiri zangu.
15Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki; nimekutafuta na nimekupata!
16Nimetandika kitanda changu kwa kitani za rangi kutoka Misri.