14“Nina sadaka za amani nyumbani; leo nimetimiza nadhiri zangu.
15Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki; nimekutafuta na nimekupata!
16Nimetandika kitanda changu kwa kitani za rangi kutoka Misri.
17Nimetia manukato kitanda changu kwa manemane, udi na mdalasini.
18Njoo, tuzame katika mapenzi mpaka asubuhi; tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi!