19Mume wangu hayupo nyumbani; amekwenda safari ya mbali.
20Amechukua mkoba uliojazwa fedha na hatakuwepo nyumbani karibuni.”
21Kwa maneno laini yule mwanamke akampotosha; alimshawishi kwa maneno yake laini.
22Mara huyo kijana alimfuata yule mwanamke kama fahali aendaye machinjoni, kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi,
23mpaka mshale umchome ini lake, kama ndege anayenaswa kwenye mtego, bila kujua itamgharimu maisha yake.