34Alisema, nzige wakaja, tunutu wasio na idadi,
35wakala kila jani katika nchi yao, wakala mazao ya ardhi yao.
36Kisha akawaua wazaliwa wote wa kwanza katika nchi yao, matunda ya kwanza ya ujana wao wote.
37Akawatoa Israeli katika nchi wakiwa na fedha na dhahabu nyingi, wala hakuna hata mmoja kutoka kabila zao aliyejikwaa.
38Misri ilifurahi walipoondoka, kwa sababu hofu ya Israeli ilikuwa imewaangukia.