36Kisha akawaua wazaliwa wote wa kwanza katika nchi yao, matunda ya kwanza ya ujana wao wote.
37Akawatoa Israeli katika nchi wakiwa na fedha na dhahabu nyingi, wala hakuna hata mmoja kutoka kabila zao aliyejikwaa.
38Misri ilifurahi walipoondoka, kwa sababu hofu ya Israeli ilikuwa imewaangukia.
39Alitandaza wingu kama kifuniko, na moto kuwamulikia usiku.
40Waliomba, naye akawaletea kware, akawashibisha kwa mkate wa mbinguni.