Zaburi 105

Waliomba, naye akawaletea kware, akawashibisha kwa mkate wa mbinguni.

Psalm 105:40 (UKJV) The people asked, and he brought quails, and satisfied them with the bread of heaven.

38Misri ilifurahi walipoondoka, kwa sababu hofu ya Israeli ilikuwa imewaangukia.

39Alitandaza wingu kama kifuniko, na moto kuwamulikia usiku.

40Waliomba, naye akawaletea kware, akawashibisha kwa mkate wa mbinguni.

41Alipasua mwamba, maji yakabubujika, yakatiririka jangwani kama mto.

42Kwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu, aliyompa Abrahamu mtumishi wake.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.