24Waliziona kazi za Bwana, matendo yake ya ajabu kilindini.
25Kwa maana alisema na kuamsha tufani iliyoinua mawimbi juu.
26Yakainuka juu mbinguni, yakashuka chini hadi vilindini, katika hatari hii ujasiri wao uliyeyuka.
27Walipepesuka na kuyumbayumba kama walevi, ujanja wao ukafikia ukomo.
28Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawatoa kwenye taabu yao.