27Walipepesuka na kuyumbayumba kama walevi, ujanja wao ukafikia ukomo.
28Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawatoa kwenye taabu yao.
29Akatuliza dhoruba kwa mnongʼono, mawimbi ya bahari yakatulia.
30Walifurahi ilipokuwa shwari, naye akawaongoza hadi bandari waliyoitamani.
31Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.