2Yuda alifanywa makao matakatifu ya Mungu, Israeli akawa milki yake.
3Bahari ilitazama ikakimbia, Yordani ulirudi nyuma,
4milima ilirukaruka kama kondoo dume, vilima kama wana-kondoo.
5Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia, nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma,
6enyi milima mkarukaruka kama kondoo dume, enyi vilima, kama wana-kondoo?