4milima ilirukaruka kama kondoo dume, vilima kama wana-kondoo.
5Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia, nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma,
6enyi milima mkarukaruka kama kondoo dume, enyi vilima, kama wana-kondoo?
7Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana, mbele za Mungu wa Yakobo,
8aliyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji, mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji.