2Kwa nini mataifa waseme, “Yuko wapi Mungu wao?”
3Mungu wetu yuko mbinguni, naye hufanya lolote limpendezalo.
4Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu, zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
5Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, zina macho, lakini haziwezi kuona;
6zina masikio, lakini haziwezi kusikia, zina pua, lakini haziwezi kunusa;