8Nitayatii maagizo yako; usiniache kabisa.
9Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani? Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.
10Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, usiniache niende mbali na amri zako.
11Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi.
12Sifa ni zako, Ee Bwana, nifundishe maagizo yako.