10Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, usiniache niende mbali na amri zako.
11Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi.
12Sifa ni zako, Ee Bwana, nifundishe maagizo yako.
13Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote zinazotoka katika kinywa chako.
14Ninafurahia kufuata sheria zako kama mtu afurahiaye mali nyingi.