Zaburi 119

Ninachukia watu wa nia mbili, lakini ninapenda sheria yako.

Psalm 119:113 (UKJV) I hate vain thoughts: but your law do I love.

111Sheria zako ni urithi wangu milele, naam ni furaha ya moyo wangu.

112Nimekusudia moyoni mwangu kuyafuata maagizo yako mpaka mwisho.

113Ninachukia watu wa nia mbili, lakini ninapenda sheria yako.

114Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu, nimeweka tumaini langu katika neno lako.

115Ondokeni kwangu, ninyi mtendao mabaya, ili niweze kushika amri za Mungu wangu!

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.